Usambazaji wa Filamu

 

Mawasiliano ya kijamii yanayopania kutoa msisimko wa kubadili jamii hautafaidi chochote ikiwa haya mawasiliano hayawafikii watu wanaolengwa. Kila mwaka, filamu za Global Dialogues zinapeperushwa kwa mamilioni ya watu kupitia kwenye tovuti na mitandao ya kijamii na televisheni. Zinapatikana kwa lugha nyingi tofauti bila malipo. Kurudufisha na kusambaza kwa hizi filamu kunaruhusiwa na kunaungwa mkono japo tu filamu haziuzwi.

Available in many languages, our films are distributed for free. Independent copying and sharing is actively encouraged, as long as the films are never sold.

Mtandao wa Intaneti: Twawashukuru Zaidi rafiki zetu walio kwenye mtandao wa YouTube kwa ushirikiana na kutuunga mkono kusio na kifani. Imedhibitika sasa kuwa filamu za Global Dialogues zimeendelea kupata umaarufu kwenye mtandao. Kila mwaka mamilioni ya watazamaji wanazipata hizi filamu kupitia huu mtandao. Filamu zote za Global Dialogues katika lugha tofauti zinapatikana kwenye hii tovuti www.youtube.com/globaldialogues. Tafadhali tunaomba ujiunge nasi kwenye hii idhaa kwa kutia sahihi yako na kutupa ishara ya kuridhika au kutoridhika kwako. Tunaomba uchangie kwa kutoa maoni yako na kusambaza hizi filamu kwa wengine wengi.

Ni rahisi na bure kuopoa hizi filamu kutoka kwenye huu mtandao. Unapo opoa filamu inayokuvutia, unaweza kuisambaza kwa urahisi kupitia kisanidi au kwenye tovuti yako.

Televisheni: Filamu zilizotengenezwa na Global Dialogues zinatolewa bila malipo kwa steshini zilizomo nchini na zinazopeperusha matangazo kwa njia ya setilaiti. Hii imewezesha watu zaidi ya 200,000,000 kufikiwa na haya matangazo ya Global Dialogues kila mwaka, kubadilisha sauti za vijana kuwa kishindo cha vijana!

Wakurugenzi wa televisheni wamependezwa na jinsi hizi filamu zimetengenezwa— ustadi wake na burudani ilioko. Umaarufu wake umeongezeka kutokana na upatikanaji wa filamu katika lugha nyingi, mada tofauti, usimulizi na ufupi wake kwa sababu hii inaziwezesha stesheni nyingi kuzipeperusha katikati ya mipangilio ya maonyesho yao. Hii ndio maana hizi filamu zimepata masaa mengi ya kutolipiwa kote ulimwenguni. Ni sharti kali la Global Dialogues kutolipa muda wa maongezi kwenye televisheni.

Mamilioni ya watazamaji kila mwaka.

Taarifa na filamu za hivi karibuni