FAQ Maswali ya Mara kwa Mara

Je, ni muda gani wa mwisho wa kuwasilisha viingilio katika mashindano ya Global Dialogues?
Ninaweza kuwasilisha kiingilio zaidi ya kimoja? Je, ninaweza kutwaa zaidi ya tuzo moja?
Mimi nina umri wa zaidi ya miaka 25 na ninataka kushiriki. Hii inawezekana?
Je, ni lazima hadithi yangu iwe inaangazia moja ya mada zilizopendekeza?
Je, ni lazima Kiingilio kiandikwe kwa Kiingereza?
Je, ni lazima niwasilishe kiingilio changu kwa njia ya kielektroniki?
Ni wakati na jinsi gani washindi watatangazwa?
Mashindano mengine ya Global Dialogues yatafanyika lini?

Je, ni muda gani wa mwisho wa kuwasilisha viingilio katika mashindano ya Global Dialogues?
Viingilio vyote ni lazima vitumwe kielektroniki au kuainishwa kwa muhuri wa posta usiku wa manane GMT tarehe Machi 31 2015.

Ninaweza kuwasilisha kiingilio zaidi ya kimoja? Je, ninaweza kutwaa zaidi ya tuzo moja?
Ndio! Unaweza kutuma viingilio vingi kadri ya uwezo wako. Na ndio, unaweza kuwa mshindi zaidi ya mara moja.

Mimi nina umri wa zaidi ya miaka 25 na ninataka kushiriki. Hii inawezekana
Ndio. Kama umri wako umepita miaka 25, unaweza kushiriki ilmuradi unafanya kazi na kikundi cha vijana walio na umri ya chini ya miaka 25. Lazima mmuteua mtu aliye chini ya miaka 25 kuwa kiongozi wa kikundi hicho.

Je, ni lazima hadithi yangu iwe inaangazia moja ya mada zilizopendekeza?
La. UNAWEZA KUANDIKA KUHUSU MADA YOYOTE UNAYOITAKA, BORA TU IWE INAHUSIANA NA Ukimwi, Ujinsia, Dhulma dhidi ya wanawake, ama ulevi wa pombe, madawa ya kulevya / mihadarati na ngono.

Je, ni lazima Kiingilio kiandikwe kwa Kiingereza?
Mwaka huu, viingilio vitakubaliwa vikiwa katika lugha rasmi ya mashindano ya Global Dialogues nazo ni: Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kichina, Kivusi au Kiswahili. Lugha nyingine zitaongezwa katika orodha hii miaka ijayo. Kama utawasilisha Kiingilio chako ukitumia lugha nyingine isiyoorodheshwa, tafadhali unaombwa uitafsiri kwanza katika mmoja ya lugha rasmi zilizo orodheshwa kabla hujawasilisha kiingilio chako.

Je, ni lazima niwasilishe kiingilio changu kwa njia ya kielektroniki?
Unaweza kuwasilisha kiingilio chako kwa njia ya kielektroniki au kupitia posta. Njia yo yote inaruhusiwa.

Ni wakati na jinsi gani washindi watatangazwa?
Baada ya tarehe ya mwisho ya mashindano, washindi watachaguliwa baada ya viingilio vyote kukaguliwa na majopo ya wataalamu. Washindi wa mashindano watatangazwa kabla ya mwisho wa Agosti kupitia mtandao wa kijamii wa Global Dialogues.

Mashindano mengine ya Global Dialogues yatafanyika lini?
Mashindano yetu sasa yatakuwa yakifanyika kila mwaka. Tafadhali jiunge nasi kwenye vyombo vya habari vya kijamii upate habari kamili.

Taarifa na filamu za hivi karibuni