Kanuni na zawadi

 

Ni Nini?

Unakaribishwa kubuni hadithi yoyote itakayotumika kuunda filamu fupi kuhusu HIV/Ukimwi, Ujinsia, Dhuluma dhidi ya wanawaka, ama ulevi wa pombe, madawa ya kulevya / mihadarati na ngono. Unaweza kubuni hadithi au pia kusimulia hadithi za kweli zenye matukio uliyopitia na unataka watu wajue. Wazo nzuri linalochaguliwa linawasilishwa kwa baadhi ya waendeshaji sinema waliobobea duniani na wanaoshirikiana na waigizaji stadi ambao wanazigeuza kuwa filamu za Global Dialogues. Katika kila filamu, jina la mwandishi linaandikwa waziwazi na hizi filamu zinawafikia zaidi ya watu 200,000,000 kwenye mtandao wa tovuti na mitandao ya kijamii na kwenye televisheni kila mwaka.

Nani na wapi?

Global Dialogues ni wazi kwa wagombeaji wote vijana ko kote ulimwenguni watakao kuwa chini ya miaka 25 mnamo Machi 31 2015. (Endapo umeitimu huu umri, unaweza kushiriki kwenye mashindano kwa kufanya kazi katika kikundi kinachoongozwa na kijana aliye chini ya miaka 25.)

Wakati?

Washindani lazima wawasilishe mawazo yao kupitia barua pepe au kupitia sanduku la posta na hii barua kunakiliwa kwa kupigwa muhuri wa posta kabla saa sita usiku GMT tarehe Machi 31 2015.

Jinsi ya kushiriki?

Ni juu yako kuamua jinsi utakavyowasilisha wazo lako. Washiriki wengi katika mashindano ya Global Dialogues huandika hadithi fupi, lakini pia unaweza kutuma wazo lako katika video, tamthilia fupi, gazeti lenye hadithi za vibonzo, wimbo au shairi. … Chochote kinawezekana bora tu uwasilishe kwa lugha rasmi ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kichina, Kivusi au Kiswahili.

Kama unaamua kuandika hadithi, unaombwa usizidishe kurasa 10. Ukirekodi wimbo au video unaombwa usipitishe dakika 10.

Unapoandika na kunakili wazo lako, tafadhali zungumza na mashirika au watu binafsi katika jamii yako ambao wanaweza kukupa habari mahsusi ya masuala unayoweza kuangazia au kutembelea tovuti zenye habari ya kuaminika.

Kila mshiriki (au kiongozi wa timu/kikundi) lazima ujaze fomu ya kidadisi cha kushiriki. Hivyo, ili kushiriki katika mashindano, ni lazima utimize mambo mawili: utume kiingilio chako na fomu ya kidadisi cha kushiriki.

Ili kuona fomu ya kidadisi cha kushiriki, anwani ambapo unaweza kutuma kiingilio chako na orodha ya mada zilizopendekezwa, tafadhali tembelea sehumu ilioanishwa Kuwasilisha Kiingilio Chako.

Haki ya Kunakili.

Mashindano ya Global Dialogues yanaratibiwa na GDT (Wakfu wa Global Dialogues, uliosajiliwa Uingereza, No 1,071,484). Viingilio vyote vya mashindano vitakuwa mali ya GDT, ambayo inahifadhi haki ya kuzichapisha kwa namna yoyote katika muktadha wa shughuli zake, kutaja jina la mwandishi (au kiongozi wa timu/kikundi) katika matumizi ya hivi viingilio. Washiriki wanawaachia GDT hakimiliki. Washindi wanawaidhinisha waandalizi kutumia majina na anuani zao kwa madhumuni ya utangazaji.