Dira au maono na dhima

 

Dira au Maono yetu: Global Dialogue inatarajia kuweko kwa dunia yenye afya bora, yenye amani, na pahali ambapo utu, huruma, kujaliana itakithiri vile vile usawa na umoja kati ya watu wa tabaka na hulka mbalimbali.

Dhima au Kazi Mahsusi Yetu: Kueneza afya na utu bora kwa jamii tukitumia mbinu zilizoingiliana, zinazoelekezwa na kutumiwa na vijana na zinazo pewa nguvu kutokana na ubunifu na kushirikisha utaalam mbalimbali.

Sifa mbalimbali za kuielezea Global Dialogues

  • wenye uadilifu
  • Wanaozingatia uwazi na ushirikiano
  • wazingatiao ubora wa hali ya juu
  • wenye tajriba pana
  • wabunifu
  • wenye kutafuta kushirikisha maono na utendakazi
  • wanoamini uwekezaji kwa jamii
  • wanao chambua miiko
  • wenye nyoyo za mapenzi
  • walio na maono mapana
  • wenye kuwapa vijana nguvu na motisha
Vijana. Wabunifu. Dira au Maono.

"Nyenje waweza kumshikilia kwenye kiganja chako, lakini mlio wake itasikika kote nyikani."

"Tandabui ikiunganika itaweza kumfungia simba."

~Methali za Kiafrika

Taarifa na filamu za hivi karibuni