Historia yetu

 

Wakati wowote tunapowasimulia watu historia ya Global Dialogues, huwa tunaanza kwa kutoa shukrani zetu za dhati kwa marafiki zetu Didier Jayle na Antonio Ugidos. Mwanzoni mwa mwaka wa 1990, hawa wawili pamoja na washirika wao wa CRIPS walifikiria na baadaye kutekeleza mradi maalum uliojulikana kama Matukio 3,000 dhidi ya Virusi. Kuhusika kwao, na jinsi walivyotekeleza majukumu yao kwa wingi wa nidhamu pamoja na kuheshimu mtazamo na mawazo ya vijana kama njia mojawapo ya kupaaza sauti zao kwa kutumia vyombo vya habari vya kijamii vyenye kupania kuleta mageuzi, ni jambo la kupongezwa mno kutokana na kuleta matokeo yanayotakiwa. Tunawashukuru Didier na Antonio kwa kutupa idhini pale mwaka wa 1997, tulipobuni Global Dialogues Trust na kuwataka kutupa msukumo kutokana na kazi yao nzuri ambayo ni mfano wa kuigwa.

Mwaka huo huo tulianzisha mradi wa majaribio kupitia wazo la Matukio 3,000 katika mataifa matatu ya Magharibi mwa Afrika. Maelfu ya vijana walishiriki mwanzoni mwa shindano la “Matukio kutoka Sahel” ambalo ni shindano la uandishi wa hadithi zinazotengeneza filamu fupi kuhusu maambukizi ya HIV/UKIMWI. Nao wataalamu wa filamu waliohusishwa wakaongezea ujuzi wao wa uliogeuzi baadhi hadithi zilizowasilishwa kuwa filamu fupi za kuvutia. Mnamo mwaka wa 2002,mradi huo ulipanuka na kuwa “Matukio kutoka Afrika”, na kwa zaidi ya miaka kumi iliyofuatia mradi huo ulipanuka zaidi na kusambaa kote barani Afrika na hata kwa baadhi ya Waafrika wanaoishi katika nchi za ngámbo. Kuanzia mwaka wa 1997 hadi 2012, zaidi ya vijana 150,000 kutoka mataifa 50 wameweza kushiriki kwenye mashindano ya Matukio yaliyoandaliwa na Global Dialogues. Zaidi ya hayo, filamu 39 zimeundwa kutokana na miswada iliyoshinda kwenye mashindano. Kila mwaka, baadhi ya filamu hizi zinatayarishwa na kutolewa katika lugha 29 na kusambazwa kwa zaidi ya watu 200,000,000. Filamu za Matukio/Global Dialogues ni baadhi ya filamu za kielimu zinazotumika zaidi katika kuielimisha jamii kote barani Afrika kuhusiana na maambukizi ya HIV/UKIMWI na filamu hizi za “Matukio kutoka Afrika” zinaweza kutazamwa kupitia anwani ifuatayo; www.youtube.com/globaldialogues.

Vipindi vyetu na mbinu zetu zimepitia mabadiliko makubwa tangu mradi wa kwanza ulipoanzishwa. Mbali na kuangazia pekee mada ya HIV/UKIMWI–, mada nyenginezo zenye umuhimu mkubwa kwa vijana na jamii zao pia zimejumuishwa. Na kutokana na maombi kutoka maeneo mbalimbali, mengine kati yao yakiwa nje ya bara la Afrika, mwishoni mwa mwaka 2012, mradi huu ulipanuliwa zaidi na kuwa wa kimataifa na kwa sasa unatumia jina la Global Dialogues— shirika linaloratibu shughuli zake.

Picha

Taarifa na filamu za hivi karibuni