Maelezo kuhusu mradi

 

Shughuli za Global Dialogues zimekuwa zikipanuka na kukua tangu mradi huu ulipoanzishwa mnamo mwaka wa 1997, na unahusisha vigezo vitano muhimu vinavyoingiliana na kuhusisha pande mbili husika kwa lengo la kuimarisha na kutilia nguvu:

Global Dialogues PROCESS photoSauti ya Vijana na Uhamasishaji wa Kijamii. Makundi ya uhamasishaji ya Global Dialogues yamekuwa yakifanya kazi mashinani na kuishirikisha jamii pamoja na kuwahusisha vijana katika kupitia mawasiliano ya mtandao kwa njia maalum ya uvumbuzi na inayowaleta vijana pamoja kama njia mojawapo ya kupaaza sauti yao. Kwenye mashindano ya kimataifa, vijana hujieleza kwa kuandaa hadithi, au kwa kutoa masimulizi ya hadithi zinazolenga mada maalum ikiwemo afya ya umma na mada nyenginezo zenye umuhimu kote ulimwenguni.

Kwa kuwa na maingiliano ya ubunifu – hadithi na masimulizi ya vijana hupewa uhai kupitia filamu za Global Dialogues na uwasilishaji wa kazi za sanaa. Filamu hizi hupatikana katika lugha mbalimbali na hutolewa bila malipo katika viwango vya jamii, kwenye mitandao na hata televisheni na huwafikia mamilioni ya watu kila mwaka.

Kupata elimu mpya na mitazamo ya vijana kupitia udadisi wa hadithi. Hadithi zinazobuniwa na vijana katika shughuli za Global Dialogues hupitiwa kwa mpangilio maalum kwa lengo la kupata fikra mpya za vijana, hisia zao, shauku, ndoto zao, changamoto na hata suluhu.

Uhamasishaji wa vitendo Mashinani na Kimataifa.  Utayarishaji wa filamu kwa usanii wa hali ya juu wa Global Dialogues pamoja na kutoa elimu mpya inayopatikana kupitia uhakiki wa masimulizi ya hadithi fupi hutumika katika kuboresha sera na program husika katika viwango mbalimbali.

Usimamaizi wa hali ya juu na uwazi wa kubadilishana mafunzo.

Katika shughuli zake zote kundi la Global Dialogues hupania kuhamasisha kuhisi maono ya mwengine, kuoneana huruma kwa lengo la kuleta usawa na umoja kwa watu mbalimbali ulimwenguni.

Taarifa na filamu za hivi karibuni