Utengenezaji wa Filamu

 

Global Dialogues inajihusisha na uzalishaji wa maonyesho ya habari inayopania kulete mabadiliko ya kijamii ili kusaidia kujenga ulimwengu wenye afya njema na amani, yenye nguzo ya kuweza kuona maono ya wengine, huruma na umoja hata tukiwa wa tabaka mbalimbali.

Filamu zetu ambazo zinachipuka kutoka kwa hadithi zinazotungwa na vijana chipukizi wabunifu wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa zinatungwa na waelekezaji wa filamu waliobobea wakishirikiana na vijana wanaoimarishs vipawa vyao. Hadi mapema 2012, filamu zetu zote ziliangazia HIV/UKIMWI na zilikuwa zinatengenezewa Afrika. Sasa Global Dialogues inaangazia ulimwengu mzima na mambo makuu yanayoyapa kipaumbele yamepanuka na kujuisha mambo mengine mengi yanayowakumba vijana kote duniani.

Hizi filamu zinathaminiwa sana na watangazaji, mashirika ya kijamii yasiyo ya kiserekali, wanaoshiriki katika harakati za uhamasishaji wa kijamii na kimataifa, shule na hata wafanyi biashara. Umaarufu wake kwenye mtandao unazidi kupanda.

Wataalamu wa filamu wa Global Dialogues daima wanazingatia kanuni zifuatazo:

  • Filamu hazitengenezwi kama chombo cha kutoa mafunzo na ujumbe tu bali kama ala ya kuchochea watazamaji kutafakari na kuzua majadiliano. Wao huonyesha imani yetu katika jamii kutambua, kuchunguza na kutatua masuala yao wenyewe waliyoyapa kipaumbele, kupitia njia yao wenyewe.
  • Filamu hazitengenezwi kama chombo cha kutoa mafunzo na ujumbe tu bali kama ala ya kuchochea watazamaji kutafakari na kuzua majadiliano. Wao huonyesha imani yetu katika jamii kutambua, kuchunguza na kutatua masuala yao wenyewe waliyoyapa kipaumbele, kupitia njia yao wenyewe.
  • Jinsi mengi mema yanaweza kufanywa na filamu iliyoundwa vyema juu ya swala lililo mwiko, uharibifu mkubwa unaweza kusababishwa kutokana na mtu ambaye hajachukua tahadhari zote muhimu kabla ya kutengeneza na kuieneza filamu. Ni kwa sababu hizi, watengenezaji wa filamu wa Global Dialogues wanasisitiza kuwa kabla filamu haijaanza kuundwa mswada wake unapigwa msasa vilivyo.
  • Ubunifu miongoni mwa washika dau: Utengenezaji wa filamu wa Global Dialogues ni wa kipekee kwani unajumuisha mambo mbalimbali, yanayoshirikisha vijana, mashirika ya kijamii na watengenezaji wa filamu.

Filamu za Global Dialogues zinasambazwa kwa wingi katika lugha nyingi tofauti, na zimetafsiriwa ili kuwawezesha wasio na uwezo wa kusikia na pia kuwanufaisha wanaojifunza lugha na waalimu pia.

“Malaika”, Guatemala, 2014.

Taarifa na filamu za hivi karibuni