Mapitio ya mashindano

 

“Ni kwa sababu nina jambo ninalotaka kusema, na vilevile nataka sauti yangu isikike!”

Hili ndilo jibu la kawaida kutoka kwa vijana wengi — zaidi ya vijana 200,000 kutoka nchi 75 — wanaoshiriki katika mashindano ya Global Dialogues, wanajibu wanapoulizwa kufafanua sababu zao za kushiriki kwenye mashindano.

Katika mashindano ya Global Dialogues, vijana kote duniani, wanazungumzia masuala kama vile HIV/ Ukimwi, Ujinsia, Dhuluma dhidi ya wanawaka, ama ulevi wa pombe, madawa ya kulevya / mihadarati na ngono, kwa kutunga hadithi zinazotengeneza filamu fupi.

Katika mashindano ya Global Dialogues, vijana kote duniani, wanazungumzia masuala kama vile HIV/UKIMWI na maswala ya kijinsia au vurugu, kwa kutunga hadithi zinazotengeneza filamu fupi.

Washiriki wanabuni hadithi au pia kusimulia hadithi za kweli za mambo waliyopitia na wanataka watu wajue. Hadithi zote zinatathminiwa na jopo la waamuzi ambao mbali na kuchagua mshindi, wanapata pia fursa ya kuelewa hisia na fikra za vijana kwa undani. Kazi muhimu kwa hili jopo ni kusikiza na kujifunza kutoka kwa vijana; kisha wanawaeleza wengine wanaotumia hii habari kutoa uamuzi.

Dhana nzuri zinazochaguliwa zinawasilishwa kwa baadhi ya waendeshaji sinema waliobobea duniani ambao wanazigeuza kuwa filamu za Global Dialogues zinazowafikia zaidi ya watu 200,000,000 kwenye mtandao wa tovuti ikiwemo mitandao ya kijamii na kwenye televisheni kila mwaka.

Sauti Zinasikika!

Ni matumaini yetu kwamba utafikiria kushiriki kwa kubuni hadithi yako mwenyewe au— kama wewe una zaidi ya miaka 24— kusaidia vijana katika juhudi zao na kueneza habari kuhusu haya mashindano ya Global Dialogues. Asante!

Stephanie Balmir wa Haiti, Mshindi wa kwanza wa mwaka 2014 wa shindano la kimataifa la global dialogues.

Taarifa na filamu za hivi karibuni